Kioo cha Lugha
Published by African Journals Online (AJOL)
- Scilit
- Linguistics & Language Studies
- Literary Theory
Publications Analysis
Publications in 2016-2026
Open Access Publications in 2016-2026
- Total Citations
- 7
- Total Publications
- 28
- Average Citations
- 0.25
- Cited Publications
- 6
- Cited Publications %
- 21.4%
- Self Citations
- 1
- Self Citations %
- 14.3%
- h5_index
- 2
- Monthly Citation Metric (MCM)
- 0.08
- Q1
- 0
- Med
- 0
- Q3
- 0
- 99%
- 2.7
- Max
- 3
- Citing Source Titles
- Citing Publishers
Latest Publications
- Open Access
- 7 October 2025
- Published by African Journals Online (AJOL) in Kioo cha Lugha
- Vol. 23 (1) , 107-122
Interpreting Kezilahabi’s Nagona and Mzingile through the Religious Thought of Mircea Eliade
The first experimental novels in Kiswahili literature were Nagona and Mzingile by Euphrase Kezilahabi, published in the early 1990s. Although both are considered revolutionary, their esoteric nature has allowed for diverse interpretations from scholars over the years. This study is another attempt to present the hidden meanings of these two enigmatic novels, employing the classic methodology of comparative literature, particularly by exploring intertextual connections. The analysis begins by identifying the factors contributing to their elusiveness. They are revealed to be two: the circular structure that results in the lack of a moral conclusion and the literary devices of increasing uncertainty. This study then attempts to interpret these factors with reference to the thoughts of the 20th-century religious scholar Mircea Eliade. Connections between Eliade and Kezilahabi are evident: Eliade‘s terminology appears in Mzingile, and Kezilahabi references Eliade‘s work multiple times in his doctoral dissertation. This study suggests the possibility that Eliade‘s thought influenced Kezilahabi at the level of conception of Nagona and Mzingile. Furthermore, it proposes a new reading of the two by drawing on Eliade‘s engagement with Indian philosophy.
- 7 October 2025
- Published by African Journals Online (AJOL) in Kioo cha Lugha
- Vol. 23 (1) , 107-122
Open AccessInterpreting Kezilahabi’s Nagona and Mzingile through the Religious Thought of Mircea Eliade

- Vol. 23 (1) , 86-106
Mbinu za Ujenzi wa Masuala ya Kiuhalisia Hakiki na Dhima zake katika Riwaya za Kichwamaji (1974) na Dunia Uwanja wa Fujo (1975)
Mtindo wa uhalisia hakiki unahusu uandishi wa kazi za fasihi ambapo masuala anuwai ya kijamii hubainishwa na mwandishi pasipo hofu yoyote. Mwandishi anapotumia mtindo huu katika uandishi wake huchambua maovu yaliyopo kwenye jamii na kuyaweka wazi bila kificho chochote. Wakati mwingine, uandishi wa namna hii huhatarisha usalama wake. Hivyo, ni waandishi wachache sana wenye uthubutu huo hasa kama maovu hayo yanawahusu wenye mamlaka moja kwa moja. Makala hii imechunguza mbinu zinazotumika kujenga masuala ya kiuhalisia hakiki katika uandishi pamoja na dhima za mtindo huo katika riwaya za Kichwamaji (1974) na Dunia Uwanja wa Fujo (1975) zilizoandikwa na Euphrase Kezilahabi. Data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya usomaji makini wa matini teule. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Uhalisia kwa kujikita katika mkabala wake wa uhalisia hakiki. Matokeo yameonesha kwamba kuna mbinu tano zinazotumika kujenga masuala ya kiuhalisia hakiki kiuandishi ambayo ni majadiliano baina ya wahusika, matendo ya wahusika, uzungumzinafsiya, sitiari na uwasilishaji dhahiri. Kwa upande mwingine, dhima za mtindo huo ni kumpambanua msanii, kumtafakarisha msomaji, kujenga jamii mpya na kuibua mambo mapya katika jamii.
- 7 October 2025
- Published by African Journals Online (AJOL) in Kioo cha Lugha
- Vol. 23 (1) , 86-106
Open AccessMbinu za Ujenzi wa Masuala ya Kiuhalisia Hakiki na Dhima zake katika Riwaya za Kichwamaji (1974) na Dunia Uwanja wa Fujo (1975)
Mtindo wa uhalisia hakiki unahusu uandishi wa kazi za fasihi ambapo masuala anuwai ya kijamii hubainishwa na mwandishi pasipo hofu yoyote. Mwandishi anapotumia mtindo huu katika uandishi wake huchambua maovu yaliyopo kwenye jamii na kuyaweka wazi bila kificho chochote. Wakati mwingine, uandishi wa namna hii huhatarisha usalama wake. Hivyo, ni waandishi wachache sana wenye uthubutu huo hasa kama maovu hayo yanawahusu wenye mamlaka moja kwa moja. Makala hii imechunguza mbinu zinazotumika kujenga masuala ya kiuhalisia hakiki katika uandishi pamoja na dhima za mtindo huo katika riwaya za Kichwamaji (1974) na Dunia Uwanja wa Fujo (1975) zilizoandikwa na Euphrase Kezilahabi. Data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya usomaji makini wa matini teule. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Uhalisia kwa kujikita katika mkabala wake wa uhalisia hakiki. Matokeo yameonesha kwamba kuna mbinu tano zinazotumika kujenga masuala ya kiuhalisia hakiki kiuandishi ambayo ni majadiliano baina ya wahusika, matendo ya wahusika, uzungumzinafsiya, sitiari na uwasilishaji dhahiri. Kwa upande mwingine, dhima za mtindo huo ni kumpambanua msanii, kumtafakarisha msomaji, kujenga jamii mpya na kuibua mambo mapya katika jamii.
- 7 October 2025
- Published by African Journals Online (AJOL) in Kioo cha Lugha
- Vol. 23 (1) , 55-66
Dhima ya Lugha ya Mhusika Mtoto katika Vichekesho Teule vya Anko Zumo
Vichekesho ni kipera cha fasihi simulizi kinachoendelea kukua na kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia. Hii inamaanisha kuwa kama ambavyo mambo mengi yamebadilika kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, sanaa ya vichekesho nayo imebadilika, hususani katika vipengele vya uhifadhi na uwasilishaji wake. Hivi sasa vichekesho vinawasilishwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, kama vile YouTube, Instagram, Facebook na Twitter. Anko Zumo ni miongoni mwa vichekesho vinavyowasilishwa kupitia mitandao ya kijamii. Vichekesho hivi hutumia wahusika watu wazima na watoto. Miongoni mwa wahusika wakuu wa vichekesho hivi ni mtoto Maisara Mohamed maarufu kama Mai Zumo. Mhusika huyu anatumia lugha ili kuivutia hadhira na kuifanya icheke. Licha ya kuivutia hadhira na kuifanya icheke, zipo tafiti mbalimbali zinazoonesha kuwa matumizi ya watoto katika kazi za sanaa hayafanyiki kiholela bali huwa na dhima anuwai. Suala hili liliibua makala hii ambayo imelenga kuchunguza dhima ya lugha ya mhusika mtoto katika vichekesho vya Anko Zumo. Data za makala hii zilipatikana kwa kuchunguza vichekesho teule tisa (9) kupitia mtandao wa YouTube. Uchambuzi wa data uliongozwa na Nadharia ya Uvunjaji wa Kanuni Usio na Madhara. Matokeo yanaonesha kuwa lugha ya mhusika mtoto katika vichekesho teule vya Anko Zumo ina dhima anuwai.

- Vol. 23 (1) , 67-85
Mikinzano ya Kimtazamo baina ya Wahusika Inavyobainisha Falsafa ya Kiafrika: Mifano kutoka Riwaya ya Dunia Uwanja wa Fujo (2007)
Tofauti za kimtazamo baina ya wahusika zimekuwa zikijitokeza katika kazi mbalimbali za riwaya. Watunzi wa kazi hizo wamekuwa na kawaida ya kuwavisha wahusika uhusika unaopambanua mawazo, imani, itikadi na falsafa mbalimbali zinazoongoza maisha yao. Kuwapo kwa mitazamo hiyo, kumechochea tafiti nyingi kuchunguza falsafa ya waandishi wa kazi hizo, mitazamo ya wahusika na uhusika wao na Uafrikanishaji wa kazi hizo, hususani za riwaya. Makala hii inalenga kuchunguza mikinzano ya kimtazamo baina ya wahusika na namna inavyobainisha falsafa ya Kiafrika. Data za utafiti zimepatikana uwandani kupitia njia ya usomaji na uchambuzi matini. Mchakato wa uchambuzi umeongozwa na Nadharia ya Ontolojia ya Kiafrika. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa mikinzano ya kimtazamo baina ya wahusika katika riwaya ya Dunia Uwanja wa Fujo (2007) imejitokeza katika masuala ya ndoa, uzazi, malezi, utamaduni na ujamaa. Vipengele hivyo ndivyo vimeibua mikinzano ya kimtazamo baina ya wahusika na kubainisha falsafa ya Kiafrika kwamba maisha ya Mwafrika yamejengwa katika kuthamini uzazi kama mhimili wa kuwapo na mwendelezo hai wa vizazi.
- 7 October 2025
- Published by African Journals Online (AJOL) in Kioo cha Lugha
- Vol. 23 (1) , 67-85
Open AccessMikinzano ya Kimtazamo baina ya Wahusika Inavyobainisha Falsafa ya Kiafrika: Mifano kutoka Riwaya ya Dunia Uwanja wa Fujo (2007)
Tofauti za kimtazamo baina ya wahusika zimekuwa zikijitokeza katika kazi mbalimbali za riwaya. Watunzi wa kazi hizo wamekuwa na kawaida ya kuwavisha wahusika uhusika unaopambanua mawazo, imani, itikadi na falsafa mbalimbali zinazoongoza maisha yao. Kuwapo kwa mitazamo hiyo, kumechochea tafiti nyingi kuchunguza falsafa ya waandishi wa kazi hizo, mitazamo ya wahusika na uhusika wao na Uafrikanishaji wa kazi hizo, hususani za riwaya. Makala hii inalenga kuchunguza mikinzano ya kimtazamo baina ya wahusika na namna inavyobainisha falsafa ya Kiafrika. Data za utafiti zimepatikana uwandani kupitia njia ya usomaji na uchambuzi matini. Mchakato wa uchambuzi umeongozwa na Nadharia ya Ontolojia ya Kiafrika. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa mikinzano ya kimtazamo baina ya wahusika katika riwaya ya Dunia Uwanja wa Fujo (2007) imejitokeza katika masuala ya ndoa, uzazi, malezi, utamaduni na ujamaa. Vipengele hivyo ndivyo vimeibua mikinzano ya kimtazamo baina ya wahusika na kubainisha falsafa ya Kiafrika kwamba maisha ya Mwafrika yamejengwa katika kuthamini uzazi kama mhimili wa kuwapo na mwendelezo hai wa vizazi.
- Open Access
- 7 October 2025
- Published by African Journals Online (AJOL) in Kioo cha Lugha
- Vol. 23 (1) , 16-36
Mazingira ya Utokeaji wa Alomofu za Utendeshi katika Lugha ya Kimalila
Makala hii inachambua alomofu za utendeshi zinazojitokeza katika vitenzi vya lugha ya Kimalila2 lengo likiwa kuchambua mazingira ya kutokea kwa alomofu za utendeshi zilizopo na chanzo cha kutokea kwake. Mbinu za uchanganuzi wa matini na hojaji zilitumika kukusanyia data zilizotumika katika utafiti huu. Aidha, Nadharia ya Umboupeo iliongoza utafiti huu. Matokeo yanaonesha kwamba alomofu za utendeshi katika lugha ya Kimalila zipo zinazotokea katika mazingira yanayotabirika na nyingine yasiyotabirika. Lugha ya Kimalila ina alomofu za utendeshi fupi na ndefu. Alomofu fupi ni {-y-} 3 na {-w-} na alomofu ndefu ni {-isy-}, {-izy-}, {-iz-}, {-iziz-}, {-ishiz-}, {-isiz-}, {-wiz-} na {-ikh-}. Alomofu hizi hutokea kutegemeana na kanuni za tangamano la irabu kama ilivyo kwa lugha nyingi za Kibantu. Sifa za mzizi na mfuatano wa utendeshi na utendea zinachochea kwa kiwango kikubwa kutokea kwa alomofu hizi za utendeshi. Mazingira ya kutokea kwa alomofu za utendeshi {-w-}, {-wiz-} na {-iziz-} yanaonesha upekee katika utokeaji wake. Makala inahitimisha kuwa kuna mazingira ya uteuzi na matumizi ya alomofu za utendeshi yanayofungwa na lugha mahususi (Kimalila), jambo linalofungua milango kwa tafiti zaidi katika lugha nyingine kiulinganisho.
- 7 October 2025
- Published by African Journals Online (AJOL) in Kioo cha Lugha
- Vol. 23 (1) , 16-36
Open AccessMazingira ya Utokeaji wa Alomofu za Utendeshi katika Lugha ya Kimalila

- Vol. 23 (1) , 37-54
Jiografia ya Binadamu kama Mtaimbo Endeshi wa Anthroposenia katika Riwaya za Bustani ya Edeni, Vipuli vya Figo, Mafuta na Walenisi
Makala hii inashughulikia jiografia ya binadamu kama mtaimbo endeshi wa anthroposenia katika riwaya za Emmanuel Mbogo: Bustani ya Edeni, Vipuli vya Figo; na za Katama Mkangi: Mafuta na Walenisi. Riwaya hizi nne zilisomwa kisha data zilitongolewa mintarafu ya kusudi la makala hii. Suala la anthroposenia lilichanganuliwa katika misingi ya kipindi ambacho taathira yake ingalipo na inaendelea kuwanda kiwakati katika maisha ya binadamu. Lengo kuu la makala hii ni kujadili namna janibu mbalimbali anazoishi na kuzitawala mwanadamu zilivyo na jukumu la kuhimili uendeshaji wa anthroposenia mbele, hususani za Afrika, tofauti na mabara mengine tajiri kama vile Uropa na Marekani. Nadharia ya Uhakikimazingira iliongoza uhakiki wa data za makala hii. Matokeo ya utafiti yanadhihirisha kwamba janibu fukara duniani huimarisha na huwa mtaimbo endeshi wa anthroposenia kuliko zile zenye ukwasi. Waandishi wamefanikiwa kudhihirisha wazi kuwa viongozi wa mataifa tajiri wanaelewa hili na hivyo wanayachafua na kuyaharibu zaidi mazingira ya mataifa fukara kuliko yao wenyewe.
- 7 October 2025
- Published by African Journals Online (AJOL) in Kioo cha Lugha
- Vol. 23 (1) , 37-54
Open AccessJiografia ya Binadamu kama Mtaimbo Endeshi wa Anthroposenia katika Riwaya za Bustani ya Edeni, Vipuli vya Figo, Mafuta na Walenisi
Makala hii inashughulikia jiografia ya binadamu kama mtaimbo endeshi wa anthroposenia katika riwaya za Emmanuel Mbogo: Bustani ya Edeni, Vipuli vya Figo; na za Katama Mkangi: Mafuta na Walenisi. Riwaya hizi nne zilisomwa kisha data zilitongolewa mintarafu ya kusudi la makala hii. Suala la anthroposenia lilichanganuliwa katika misingi ya kipindi ambacho taathira yake ingalipo na inaendelea kuwanda kiwakati katika maisha ya binadamu. Lengo kuu la makala hii ni kujadili namna janibu mbalimbali anazoishi na kuzitawala mwanadamu zilivyo na jukumu la kuhimili uendeshaji wa anthroposenia mbele, hususani za Afrika, tofauti na mabara mengine tajiri kama vile Uropa na Marekani. Nadharia ya Uhakikimazingira iliongoza uhakiki wa data za makala hii. Matokeo ya utafiti yanadhihirisha kwamba janibu fukara duniani huimarisha na huwa mtaimbo endeshi wa anthroposenia kuliko zile zenye ukwasi. Waandishi wamefanikiwa kudhihirisha wazi kuwa viongozi wa mataifa tajiri wanaelewa hili na hivyo wanayachafua na kuyaharibu zaidi mazingira ya mataifa fukara kuliko yao wenyewe.
- Open Access
- 7 October 2025
- Published by African Journals Online (AJOL) in Kioo cha Lugha
- Vol. 23 (1) , 1-15
Uchunguzi wa Mbinu na Vifaa vya Kufundishia Utamaduni wa Lugha ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Burundi
Makala hii imelenga kuchunguza mbinu na vifaa mbalimbali vinavyotumiwa na walimu kufundishia utamaduni wa Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Burundi. Katika ukusanyaji wa data, hojaji na ushuhudiaji ndizo mbinu zilizotumiwa. Nadharia ya Utamaduni-Jamii ya Vygostsky (1980) ilitumika katika uchanganuzi wa data. Data ilichambuliwa kwa kutumia majedwali, maelezo na programu tumizi ya kuchambua data ya SPSS (Statistical Package for the Social Sciences). Matokeo yameonesha kuwa baadhi ya walimu wa Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Burundi wanaingiza masuala ya utamaduni katika ufundishaji na wanatumia mbinu tano katika ufundishaji wao. Hata hivyo, matokeo yameonesha kwamba mbinu mbili ambazo ni uigizaji na majadiliano kuhusu vitabu na matini za Kiswahili ndizo zinazotumiwa kwa kiwango kikubwa. Kuhusu vifaa vya kufundishia masuala ya utamaduni wa Kiswahili, utafiti huu umedhihirisha kuwa vitabu, intaneti, projekta na kompyuta ndivyo vifaa vinavyotumiwa kwa asilimia kubwa. Walimu wameshauriwa kubuni mbinu na vifaa vinavyoweza kuwasaidia kufanikisha mafunzo ya utamaduni wa Kiswahili kwa sababu lugha na utamaduni havitenganishwi.
- 7 October 2025
- Published by African Journals Online (AJOL) in Kioo cha Lugha
- Vol. 23 (1) , 1-15
Open AccessUchunguzi wa Mbinu na Vifaa vya Kufundishia Utamaduni wa Lugha ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Burundi
Makala hii imelenga kuchunguza mbinu na vifaa mbalimbali vinavyotumiwa na walimu kufundishia utamaduni wa Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Burundi. Katika ukusanyaji wa data, hojaji na ushuhudiaji ndizo mbinu zilizotumiwa. Nadharia ya Utamaduni-Jamii ya Vygostsky (1980) ilitumika katika uchanganuzi wa data. Data ilichambuliwa kwa kutumia majedwali, maelezo na programu tumizi ya kuchambua data ya SPSS (Statistical Package for the Social Sciences). Matokeo yameonesha kuwa baadhi ya walimu wa Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Burundi wanaingiza masuala ya utamaduni katika ufundishaji na wanatumia mbinu tano katika ufundishaji wao. Hata hivyo, matokeo yameonesha kwamba mbinu mbili ambazo ni uigizaji na majadiliano kuhusu vitabu na matini za Kiswahili ndizo zinazotumiwa kwa kiwango kikubwa. Kuhusu vifaa vya kufundishia masuala ya utamaduni wa Kiswahili, utafiti huu umedhihirisha kuwa vitabu, intaneti, projekta na kompyuta ndivyo vifaa vinavyotumiwa kwa asilimia kubwa. Walimu wameshauriwa kubuni mbinu na vifaa vinavyoweza kuwasaidia kufanikisha mafunzo ya utamaduni wa Kiswahili kwa sababu lugha na utamaduni havitenganishwi.
- 11 March 2025
- Published by African Journals Online (AJOL) in Kioo cha Lugha
- Vol. 22 (2) , 229-246
Uchanganyaji Msimbo katika Jamiilugha za Mitandaopepe:Mtagusano wa Kiswahili na Kiingereza
Mitandaopepe2 imetoa fursa kwa watu kutagusana katika masuala anuwai ya kijamii. Kiswahili ni miongoni mwa lugha zinazotumiwa katika mitandaopepe, ndani na nje ya Tanzania. Kutokana na kukua na kusambaa kwa lugha hiyo ulimwenguni kote, kuna haja ya kuchunguza mwonekano wake katika muktadha huo wa kimawasilianopepe. Lengo la makala hii ni kuchunguza jinsi Kiswahili kinavyotagusana na lugha ya Kiingereza katika mawasiliano hayo, hususani kwenye kipengele cha uchanganyaji msimbo. Data za utafiti huu ni maoni yaliyotolewa kwenye mtandao wa YouTube baada ya watu kusikiliza hotuba za Kiswahili za Mwalimu Nyerere. Jumla ya maoni elfu mbili na sitini yalikusanywa kutoka katika hotuba tatu. Uchanganuzi wa data hizo uliongozwa na Kiolezo cha Myers-Scotton (2001) kinachohusu lugha msingi na lugha changiaji katika kipengele cha uchanganyaji msimbo. Matokeo ya utafiti yamedhihirisha kwamba lugha za Kiswahili na Kiingereza zinakamilishana katika muktadha wa kimawasilianopepe. Katika miktadha tofautitofauti, lugha mojawapo imetumiwa kuwa msingi wa mawasiliano huku nyingine ikijaliza sarufi ya lugha msingi. Wakati mwingine, lugha zote mbili zimetumiwa kwa pamoja huku kila moja ikijikamilisha kisarufi.

- Vol. 22 (2) , 196-210
Mabadiliko ya Utambulisho wa Mwanamke na Uimarishaji wa Ujinsuke: Mifano kutoka Riwaya ya Nyuso za Mwanamke (Mohamed, 2010)
Tafiti mbalimbali kuhusu riwaya ya Kiswahili zinaonesha kuwa mwanamke amesawiriwa kwa mitazamo mbalimbali, ukiwamo mtazamo hasi. Usawiri wa mtazamo huo unamtambulisha mwanamke kama kiumbe dhaifu na duni. Kwa kuongozwa na Nadharia ya Udenguzi, makala imeonesha namna mhusika mwanamke anavyoweza kubadilisha utambulisho hasi na kujenga utambulisho chanya. Makala imetumia data kutoka katika riwaya ya Nyuso za Mwanamke (Mohamed, 2010) zilizopatikana kwa usomaji makini. Makala imeweka bayana nafasi ya riwaya ya Kiswahili katika kujenga utambulisho wa mwanamke unaoimarisha ujinsuke2 . Matokeo haya yanatokana na uumbaji wa wahusika wanawake wanaodengua kaida za jamii zinazomkandamiza mwanamke na kufichua mbinu zinazotumiwa na baadhi ya wanajamii kuendeleza ukandamizaji huo. Pia, umuhimu wa wanawake kujitambua na kujisimamia umewekwa bayana.

- Vol. 22 (2) , 292-309
Michakato ya Kisintaksia ya Uundaji wa Sentensi Changamani za Kiswahili
Makala hii inalenga kuchambua michakato ya kisintaksia ya uundaji wa sentensi changamani za Kiswahili kwa kubainisha namna kishazi kikuu na kishazi bebwa vinavyowekwa pamoja kuunda sentensi hizo. Ili kufanikisha lengo hilo, makala imeongozwa na Nadharia Rasmi ya Chomsky (1965). Data za makala hii ni sentensi changamani za Kiswahili ambazo zilikusanywa kwa njia ya usomaji wa matini kutoka katika riwaya na magazeti. Matini hizi ziliteuliwa kwa kutumia mbinu ya usampulishaji nasibu sahili. Uchambuzi wa data ulifanyika kwa mkabala wa kitaamuli kwa kutumia mbinu ya uchambuzi wa kimaudhui. Makala hii imebaini kwamba kuna michakato mitatu inayotumika kuunda sentensi changamani ambayo ni uchopekaji, udondoshaji-chopezi na udondoshaji-chopezi hamishi. Kwa kutumia Nadharia Rasmi, imebainika kwamba kila mchakato una hatua zake katika kuunda sentensi changamani.