East African Journal of Swahili Studies
Published by East African Nature and Science Organization
- Scilit
Publications Analysis
Publications in 2016-2026
Open Access Publications in 2016-2026
- Total Citations
- 11
- Total Publications
- 99
- Average Citations
- 0.11
- Cited Publications
- 11
- Cited Publications %
- 11.1%
- Self Citations
- 10
- Self Citations %
- 90.9%
- h5_index
- 1
- Monthly Citation Metric (MCM)
- 0.03
- Q1
- 0
- Med
- 0
- Q3
- 0
- 99%
- 1
- Max
- 1
- Citing Source Titles
- Citing Publishers
Latest Publications
- Open Access
- 25 November 2026
- Published by East African Nature and Science Organization in East African Journal of Swahili Studies
- Vol. 9 (4) , 8-22
Upambanuzi wa Mchakato wa Upimaji wa Stadi ya Kuzungumza Kiswahili katika Gredi ya Sita Nchini Kenya
Stadi ya kuzungumza ni mojawapo ya umilisi wa kimsingi uliopewa kipaumbele katika Mtaala wa Umilisi (MU) Kenya ikizingatiwa kuwa nguzo muhimu ya mawasiliano na ushirikiano. Utafiti huu ulilenga kutathmini upimaji wa Stadi ya Kuzungumza Kiswahili katika Gredi ya Sita (G6) nchini Kenya, hususan kupambanua mchakato wa upimaji wake, ukiongozwa na Nadharia ya Mawasiliano ya Dell Hymes (1960). Ulitumia mkabala mseto na muundo wa Usorovea Fafanuzi, ukifanyika katika kaunti nne za magharibi mwa Kenya. Watafitiwa walikuwa walimu wa G6 kutoka shule za msingi zilizoteuliwa kwa usampulishaji makusudi, huku sampuli lengwa ikiwa walimu 355. Kati yao, hojaji 341 (asilimia 96%) zilijazwa kikamilifu na kutumika katika uchanganuzi. Data zilikusanywa kupitia uchunzaji darasani, mahojiano na uchanganuzi wa nyaraka, kisha zikachanganuliwa kiidadi (umaratokezi na asilimia) na kithamano kwa kunukuu, kutafsiri na kusarifu dhamira mbalimbali. Matokeo yanaonyesha kwamba asilimia kubwa ya walimu walihudhuria warsha za Kiswahili za MU zilizoshughulikia matamshi, fasihi simulizi, mijadala, michezo ya kuigiza na mbinu za upimaji, jambo lililowawezesha kubainisha vipengele vinavyowaondolea wanafunzi hofu ya kuzungumza na kuwajengea umilisi wa lugha. Kwa jumla, matokeo ya utafiti yalibaini kuwa mchakato wa upimaji ulionekana kuwa na msingi imara wa vigezo vya KICD, mbinu za kutathmini na nyaraka za kufundishia, ingawa unakabiliwa na changamoto za utekelezaji. Utafiti unapendekeza uwekezaji zaidi katika zana za kidijitali na matumizi ya upimaji wa kirika, ambapo wanafunzi hutathmini ufasaha wa wenzao, hatua itakayopunguza shinikizo la kuhukumiwa na mwalimu pekee
- 25 November 2026
- Published by East African Nature and Science Organization in East African Journal of Swahili Studies
- Vol. 9 (4) , 8-22
Open AccessUpambanuzi wa Mchakato wa Upimaji wa Stadi ya Kuzungumza Kiswahili katika Gredi ya Sita Nchini Kenya

- Vol. 9 (4) , 1-7
Uhusiano kati ya Mbinu za Ujifunzaji na Viwango vya Umilisi wa Msamiati wa Kiswahili Miongoni mwa Wanafunzi wa Shule za Msingi katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Tanzania.
Makala hii inachunguza mwelekeo wa uhusiano kati ya mbinu za ujifunzaji na viwango vya umilisi wa msamiati wa Kiswahili miongoni mwa wanafunzi wa shule za msingi. Utafiti ulifanyika katika shule nane za Kata za Tandika na Mbagala, Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, kwa kutumia uchunguzi kifani elezi na mkabala wa mbinu mseto. Wanafunzi 119 wa Darasa la Nne na la Saba waliainishwa kwa kuzingatia mbinu kuu waliyoripoti kutumia: mjadala, kukariri, utambuzi au ishara. Viwango vya umilisi vililinganishwa kwa mgawanyo wa madaraja A–E na wastani wa alama zenye uzito, ambapo A=5 hadi E=1. Mjadala ulikuwa na uwiano mkubwa zaidi wa Daraja A (52.78%), ilhali kukariri kulikuwa na wastani wa juu zaidi (4.18) na uwiano mkubwa zaidi wa madaraja A na B kwa pamoja (79.41%). Mjadala ulipata wastani wa 4.11; utambuzi 3.44; na ishara 2.47. Mwelekeo huu unaonesha kuwa mjadala na kukariri viliambatana zaidi na viwango vya juu vya umilisi kuliko utambuzi na ishara. Kwa kuzingatia Piaget na Krashen, matokeo yanaweza kufasiriwa kwa nafasi ya uchakataji wa maana, marudio, ingizo linaloeleweka na matumizi ya msamiati katika muktadha. Hata hivyo, uchambuzi haukutumia kipimo inferensia kama Spearman au chi-square; hivyo, matokeo ni ya kimaelezo na hayathibitishi umuhimu wa kitakwimu wala usababishaji. Makala inapendekeza uoanishaji wa data za kila mwanafunzi na matumizi ya vipimo stahiki katika tafiti zijazo.
- 25 November 2026
- Published by East African Nature and Science Organization in East African Journal of Swahili Studies
- Vol. 9 (4) , 1-7
Open AccessUhusiano kati ya Mbinu za Ujifunzaji na Viwango vya Umilisi wa Msamiati wa Kiswahili Miongoni mwa Wanafunzi wa Shule za Msingi katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Tanzania.
Makala hii inachunguza mwelekeo wa uhusiano kati ya mbinu za ujifunzaji na viwango vya umilisi wa msamiati wa Kiswahili miongoni mwa wanafunzi wa shule za msingi. Utafiti ulifanyika katika shule nane za Kata za Tandika na Mbagala, Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, kwa kutumia uchunguzi kifani elezi na mkabala wa mbinu mseto. Wanafunzi 119 wa Darasa la Nne na la Saba waliainishwa kwa kuzingatia mbinu kuu waliyoripoti kutumia: mjadala, kukariri, utambuzi au ishara. Viwango vya umilisi vililinganishwa kwa mgawanyo wa madaraja A–E na wastani wa alama zenye uzito, ambapo A=5 hadi E=1. Mjadala ulikuwa na uwiano mkubwa zaidi wa Daraja A (52.78%), ilhali kukariri kulikuwa na wastani wa juu zaidi (4.18) na uwiano mkubwa zaidi wa madaraja A na B kwa pamoja (79.41%). Mjadala ulipata wastani wa 4.11; utambuzi 3.44; na ishara 2.47. Mwelekeo huu unaonesha kuwa mjadala na kukariri viliambatana zaidi na viwango vya juu vya umilisi kuliko utambuzi na ishara. Kwa kuzingatia Piaget na Krashen, matokeo yanaweza kufasiriwa kwa nafasi ya uchakataji wa maana, marudio, ingizo linaloeleweka na matumizi ya msamiati katika muktadha. Hata hivyo, uchambuzi haukutumia kipimo inferensia kama Spearman au chi-square; hivyo, matokeo ni ya kimaelezo na hayathibitishi umuhimu wa kitakwimu wala usababishaji. Makala inapendekeza uoanishaji wa data za kila mwanafunzi na matumizi ya vipimo stahiki katika tafiti zijazo.
- Open Access
- 3 October 2026
- Published by East African Nature and Science Organization in East African Journal of Swahili Studies
- Vol. 9 (3) , 500-515
Mabadiliko katika Muundo na Maumbo katika Riwaya Teule za Kipelelezi za Kiswahili: 1957-2018
Riwaya za kipelelezi zimefanyiwa uchanganuzi huku uzingativu mwingi ukiwekwa kwenye kipengele cha uforensiki, mtindo na ploti (taz. Kamau, 1992, Ngugi, 2016 na Kombo, 2018). Tafiti hizi za awali zimedhihirisha kuchunguza kipengele kimoja kwa upekee bila kuzingatia uwiano wa vipengele vyenyewe katika riwaya za kipelelezi. Hili lilichochea kuwepo kwa haja ya kuchunguza utangamano wa vipengele vya kimuundo na mabadiliko yake katika riwaya teule za Kiswahili za kutoka mwaka wa 1957-2018. Utafiti basi umechanganua mabadiliko na maendeleo ya vipengele vya kimuundo katika riwaya teule za kipelelezi za Kiswahili za kutoka mwaka wa 1957-2018 (za karne ya 20 na za karne ya 21). Riwaya zilizoteuliwa katika utafiti huu ni za kutoka mwaka wa 1957 hadi wa 2000 (za karne ya 20) Mizimu ya Watu wa Kale (Abdalla, 1957), Simu ya Kifo (Katalambula, 1965), Mpelelezi na Genge la Wezi (Levi, 1975) na zile za kutoka mwaka wa 2001 hadi wa 2018 (za karne ya 21). Mkononi mwa Nunda (Mtobwa, 2011), Msako 1 (Sudi, 2016) na Msako 2 (Sudi, 2016). Riwaya hizi ziliteuliwa kimaksudi kwa kuzingatia kipengele cha muundo na wakati. Katika makala hii, muundo ulichunguzwa kwa undani kwa kuzingatia vipengele vya muundo ambavyo ni wahusika, maudhui na ploti. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Umuundo iliyoasisiwa na Ferdinand De Saussure (1906) katika tawi la isimu. Baadaye, nadharia hii ilitumika na Vladimir Propp (1928) na kuendelezwa na Levi-Strauss (1963) aliyeibuka na wazo kwamba Umuundo unaweza kutumika kuchanganua sayansi za kijamii ikiwemo fasihi. Kuna waitifaki wa hivi karibuni kama vile Stanton (2007) ambaye anaegemea zaidi tawi la kifasihi. Mhimili mkuu uliotuongoza ni kuwa, vipengele vya kimuundo; wahusika, maudhui na ploti huchangiana na kukamilishana. Aidha, wazo la Jakobson (1960) kuwa lugha ya kifasihi hukua na kubadilika kulingana na mabadiliko ya kijamii, kitamaduni na ya kiteknolojia lilituongoza katika kuchunguza mabadiliko na maendeleo ya muundo wa riwaya teule za kipelelezi. Utafiti huu ulikuwa wa kimaktaba ambapo mtafiti alisoma riwaya teule, makala, vitabu na kusakura mtandao ili kukusanya data inayofaa na kupata uelewa mpana wa mada. Matokeo yalionyesha kwamba, ingawa kuna ufomyula katika muundo wa riwaya za kipelelezi, kuna mabadiliko yanayodhihirika kiwakati. Riwaya za kutoka mwaka wa 2000-2018 (za karne ya 21) zimeonyesha mabadiliko kutoka kwa zile za kutoka mwaka wa 1957-2000 (za karne ya 20) katika misingi ya vipengele vya muundo ambavyo ni: usawiri wa mhusika mpelelezi mkuu, mhusika mkinzani na wa kike, mabadiliko ya kimaudhui, kiploti, kiteknolojia na kimandhari.
- 3 October 2026
- Published by East African Nature and Science Organization in East African Journal of Swahili Studies
- Vol. 9 (3) , 500-515
Open AccessMabadiliko katika Muundo na Maumbo katika Riwaya Teule za Kipelelezi za Kiswahili: 1957-2018

- Vol. 9 (3) , 561-579
Muundo na Maumbo Tangamano katika Riwaya za Kipelelezi za Kiswahili: 1957—2018
Makala hii inalenga kuchanganua muundo na maumbo tangamano ya riwaya teule za kipelelezi za Kiswahili za kutoka 1957-2018. Tafiti za awali (kama vile utafiti wa Ngugi, 2016) zimedhirihisha kuchunguza kipengele kimoja kwa upekee bila kuzingatia uwiano wa vipengele vyenyewe katika riwaya za kipelelezi. Hili lilichochea kuwepo kwa haja ya kuchunguza utangamano wa muundo na maumbo katika riwaya teule kutoka 1957-2018. Katika kazi hii, muundo ulichunguzwa kwa undani kwa kuzingatia vipengele vya muundo kama vile: wahusika, maudhui, ploti, na mandhari. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Umuundo iliyoasisiwa Ferdinand De Saussure (1906) katika tawi la isimu. Baadaye, nadharia hii ilitumika na Propp (1928) na kuendelezwa na Levi-Strauss (1946) aliyeibuka na wazo kwamba nadharia hii inaweza kutumika kuchanganua sayansi za kijamii ikiwemo fasihi. Kuna waitifaki wa hivi karibuni kama vile Barthes (1977), Culler (1975), Scholes na Stanton (2007) ambaye anaegemea zaidi tawi la kifasihi. Stanton (2007) anaamini kwamba nadharia ya umuundo ni muhimu sana katika kuhakiki riwaya. Mhimili mkuu uliotuongoza ni kuwa vipengele vya kimuundo; wahusika, maudhui. Ploti na mandhari huchangiana na kukamilishana. Aidha, wana umuundo waliamini kuwa sheria ya umuundo hushughulikia zaidi muingiliano bali siyo utengano. Utafiti huu ulikuwa wa kimaktaba ambapo mtafiti alijukumika kusoma riwaya teule ili kupata data ya kimsingi. Data ya upili ilipatikana kwa kusoma makala na vitabu. Aidha, sampuli iliteuliwa kwa kutumia mbinu ya usampulishaji wa kimaksudi ambapo riwaya teule ziliteuliwa kimaksudi kwa kuzingatia kipengele cha muundo na wakati, yaani zile zilizoandikwa karne ya 19 na zile za karne ya 20. Riwaya zilizoteuliwa katika utafiti huu za kutoka mwaka wa 1957 hadi wa 2000 (za karne ya 20) Mizimu ya Watu wa Kale (Abdalla, 1957), Simu ya Kifo (Katalambula, 1965), Mpelelezi na Genge la Wezi (Levi, 1975) na zile za kutoka mwaka wa 2001 hadi wa 2018 (za karne ya 21) Mkononi mwa Nunda (Mtobwa, 2011), Msako 1 (Sudi, 2016) na Msako 2 (Sudi, 2016). Riwaya hizi ziliteuliwa kwa kuwa za karne ya 20 zina data hitajika ya vipengele vya kimuundo vilevile za karne ya 21 zinaonyesha utangamano wa kimuuundo na vile vya karne ya 20. Matokeo yalionyesha kuwa riwaya za kipelelezi za Kiswahili zilizoandikwa kutoka mwaka wa 1957-2018 zilisawiri utangamano kwa kiwango kikubwa katika vipengele vyote vya kimuundo. Kama riwaya zingine za kipelelezi, ufomyula unadhihirika katika vipengele vyote vya kimuundo ambavyo ni wahusika, ploti maudhui na mandhari. Kwa mfano kuna jukumu la mpelelezi maalum, kama mhusika mkuu mwenye sifa bainifu, linalojitokeza katika riwaya zote sita. Fauka ya hayo, miisho ya riwaya zote teule zilidhihirisha urejesho wa utulivu; Wema kushinda uovu
- 3 October 2026
- Published by East African Nature and Science Organization in East African Journal of Swahili Studies
- Vol. 9 (3) , 561-579
Open AccessMuundo na Maumbo Tangamano katika Riwaya za Kipelelezi za Kiswahili: 1957—2018

- Vol. 9 (3) , 472-484
Namna Mtindo Unavyotumika na Mwandishi katika Kuwasilisha Maudhui ya Kifo Kwenye Riwaya ya Chozi la Heri
Utafiti huu ulichunguza namna mtindo unavyotumiwa na mwandishi katika kuwasilisha maudhui ya kifo katika riwaya ya Chozi la Heri (2014) ya Assumpta K. Matei. Mtindo ni kipengele muhimu cha kisanaa kinachomwezesha mwandishi kuwasilisha maudhui kwa namna ya kipekee na yenye mvuto kwa wasomaji. Katika kazi za fasihi, maudhui ya kifo yanaweza kuwasilishwa kupitia uteuzi wa lugha na matumizi ya mbinu mbalimbali za kimtindo zinazosaidia kujenga taswira, kuibua hisia na kusisitiza ujumbe unaokusudiwa. Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Umitindo kwa mujibu wa Leech (2013), iliyowezesha kuchunguza uteuzi wa lugha na mbinu za kisanaa zinazotumiwa na mwandishi katika kuwasilisha maudhui ya kifo. Muundo wa utafiti uliotumika ni wa kimaelezo. Eneo la utafiti ni fasihi ya Kiswahili, huku sampuli ya utafiti ikiwa riwaya ya Chozi la Heri (2014), iliyoteuliwa kimakusudi kutokana na namna inavyoshughulikia maudhui ya kifo. Data zilikusanywa kupitia usomaji makini wa riwaya teule zaidi ya mara moja na kunakili vifungu vilivyohusiana na matumizi ya mtindo katika kuwasilisha maudhui ya kifo. Data hizo zilichanganuliwa kimaelezo kwa kuzingatia mhimili wa nadharia ulioteuliwa. Matokeo ya utafiti yalibainisha kuwa mwandishi alitumia mbinu mbalimbali za kimtindo zikiwemo tashbihi, tashihisi, methali, nahau na tafsida katika kuwasilisha maudhui ya kifo. Utafiti ulihitimisha kuwa mtindo una nafasi muhimu katika kuwasilisha na kuimarisha maudhui ya kifo katika riwaya ya Chozi la Heri (2014), kwani matumizi ya lugha na mbinu mbalimbali za kisanaa yanamwezesha mwandishi kuibua hisia, kujenga taswira na kufikisha ujumbe kwa ufanisi zaidi. Matokeo ya utafiti huu yanatarajiwa kuwa na manufaa kwa wanafunzi, walimu, wahakiki na wanazuoni wa fasihi ya Kiswahili kwa kupanua maarifa kuhusu mchango wa mtindo katika uwasilishaji wa maudhui ya kifo katika kazi za fasihi.
- 3 October 2026
- Published by East African Nature and Science Organization in East African Journal of Swahili Studies
- Vol. 9 (3) , 472-484
Open AccessNamna Mtindo Unavyotumika na Mwandishi katika Kuwasilisha Maudhui ya Kifo Kwenye Riwaya ya Chozi la Heri

- Vol. 9 (3) , 462-471
Aina za Lugha Zinazotumika katika Mawasiliano Kati ya Wataalamu wa Lishe na Wagonjwa: Utafiti wa Hospitali Kuu ya Thika, Kenya
Katika utoaji wa huduma za afya, lugha ni nyenzo muhimu inayowezesha mawasiliano bora kati ya wataalamu wa afya na wagonjwa. Mawasiliano yenye ufanisi husaidia katika utoaji wa taarifa sahihi, uelewa wa maelekezo ya kitabibu na kuboresha ubora wa huduma za afya. Tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa lugha inayotumika katika mazingira ya afya huathiri namna taarifa zinavyowasilishwa, kueleweka na kutekelezwa na wagonjwa. Utafiti huu ulichunguza aina za lugha zinazotumika katika mawasiliano kati ya wataalamu wa afya na wagonjwa katika Hospitali Kuu ya Thika. Pia ulilenga kubaini sababu zinazoathiri matumizi ya lugha, changamoto zinazojitokeza na athari za lugha katika uelewa wa wagonjwa. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Sajili na Nadharia ya Umitindo. Nadharia ya Sajili inaeleza kuwa matumizi ya lugha hutegemea muktadha wa mawasiliano, mazingira na mahitaji ya washiriki. Nadharia ya Umitindo inaonyesha kuwa wazungumzaji hubadili mtindo wa lugha kulingana na hali, hadhira na madhumuni ya mawasiliano. Nadharia hizi zilisaidia kueleza namna wataalamu wa afya huchagua lugha wanapowasiliana na wagonjwa. Utafiti ulitumia muundo wa mbinu mseto uliounganisha mbinu za kiasi na ubora. Data zilikusanywa kwa kutumia hojaji na mahojiano kutoka kwa wagonjwa na wataalamu wa afya katika Hospitali Kuu ya Thika. Sampuli ilijumuisha wagonjwa arobaini (40) na wataalamu wa afya watano (5) walioteuliwa kwa kutumia usampulishaji nasibu. Uhalali wa vifaa vya utafiti ulithibitishwa kwa kutumia Cronbach Alpha, ambapo kiwango cha 0.82 kilionyesha utegemezi wa vifaa hivyo.Data zilichanganuliwa kwa kutumia SPSS kwa data za kiasi na uchanganuzi wa mada kwa data za ubora. Matokeo yalionyesha kuwa Kiswahili ndicho lugha iliyotumika zaidi katika mawasiliano kati ya wataalamu wa afya na wagonjwa, kikifuatiwa na Kiingereza na lugha za kienyeji. Utafiti ulibaini kuwa matumizi ya lugha rahisi huongeza uelewa wa wagonjwa, ilhali istilahi ngumu za kitabibu na tofauti za lugha husababisha changamoto. Utafiti unapendekeza matumizi ya lugha rahisi, mafunzo ya mawasiliano kwa wataalamu wa afya, matumizi ya wakalimani na tafiti zaidi kuhusu matumizi ya lugha katika hospitali nyingine nchini Kenya.
- 3 October 2026
- Published by East African Nature and Science Organization in East African Journal of Swahili Studies
- Vol. 9 (3) , 462-471
Open AccessAina za Lugha Zinazotumika katika Mawasiliano Kati ya Wataalamu wa Lishe na Wagonjwa: Utafiti wa Hospitali Kuu ya Thika, Kenya

- Vol. 9 (3) , 441-461
Misemo ya Kidini Iliyopo kwenye Magari na Ukuzaji wa Kiswahili Mpakani Mutukula Wilayani Kyotera, Uganda
Utafiti huu ulilenga kuchunguza mchango wa misemo ya kidini iliyopo kwenye magari mpaka wa Mutukula wilayani Kyotera katika kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili miongoni mwa wananchi. Malengo mahususi ya utafiti huu ni kuchambua misemo ya kidini inayopatikana kwenye magari katika matumizi ya Kiswahili pamoja na athari zake katika maadili ya kijamii na mawasiliano ya kila siku. Utafiti huu ulitumia muundo wa kimaelezo. Data zilikusanywa kupitia mbinu za uchunguzi wa moja kwa moja, dodoso, na mahojiano. Walengwa wa utafiti walikuwa madereva wa magari ya usafiri wa umma, wamiliki wa magari, abiria na wakazi wa eneo la mpakani pamoja na viongozi wa dini. Sampuli ya jumla ya washiriki 25 ilitumika, na walichaguliwa kwa kutumia mbinu ya uteuzi wa usampulishaji. Data za kimaelezo zilichambuliwa kwa kutumia mbinu ya uchambuzi wa mada, ilhali data za kiasi zilichambuliwa kwa kutumia asilimia na takwimu rahisi. Matokeo ya utafiti yalionesha kuwa misemo ya kidini kwenye magari ina mchango mkubwa katika kukuza matumizi ya Kiswahili. Ilibainika kuwa misemo hiyo inatumika kama njia ya mawasiliano ya kijamii, ilipanua msamiati wa Kiswahili, na kuimarisha matumizi ya lugha fasaha miongoni mwa wananchi. Misemo hiyo inasaidia kuhamasisha maadili mema kama vile upendo, amani, uvumilivu na heshima katika jamii ya mpakani. Utafiti ulipendekeza kuwa misemo hiyo iandaliwe kwa Kiswahili sanifu, ihusishe wataalamu wa lugha na viongozi wa dini, na itumike kama nyenzo ya kufundishia na kukuza Kiswahili katika jamii. Aidha, serikali na taasisi za lugha zilihimizwa kuunga mkono matumizi ya maandishi ya umma yenye ubora ili kuimarisha lugha na maadili ya kijamii. Kwa ujumla, utafiti ulihitimisha kuwa misemo ya kidini kwenye magari ni nyenzo muhimu ya kijamii na kiisimu inayochangia kwa kiasi kikubwa kukuza Kiswahili, kuimarisha mawasiliano na kudumisha maadili katika jamii ya mpakani Mutukula.
- 3 October 2026
- Published by East African Nature and Science Organization in East African Journal of Swahili Studies
- Vol. 9 (3) , 441-461
Open AccessMisemo ya Kidini Iliyopo kwenye Magari na Ukuzaji wa Kiswahili Mpakani Mutukula Wilayani Kyotera, Uganda

- Vol. 9 (3) , 428-440
Athari za Ujumi wa Kiafrika katika Ujenzi wa Mhusika wa Kike katika Tamthiliya ya Nguzo Mama
Makala hii imefafanua athari za ujumi wa Kiafrika katika ujenzi wa wahusika wa kike katika tamthiliya ya Nguzo Mama ya Penina Muhando. Lengo lilikuwa kubainisha namna vipengele vya ujumi wa Kiafrika vinavyoathiri utambulisho nafasi, sauti, uwezo, mahusiano na taswira za wahusika wa kike. Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Ujumi wa Kiafrika, inayosisitiza uhusiano wa sanaa na maisha, maadili, mazingira, ushirikiano na tajiriba za jamii. Utafiti ulitumia mkabala wa kitaamuli na usanifu wa kifani. Data zilikusanywa kupitia usomaji makini wa tamthiliya iliyoteuliwa, usaili na majadiliano ya vikundi. Washiriki walikuwa 15, wakiwamo wahadhiri watatu wa fasihi ya Kiswahili na wanafunzi 12 waliokuwa na maarifa kuhusu tamthiliya hiyo. Washiriki waliteuliwa kwa usampulishaji lengwa na data zilichambuliwa kwa mkabala wa kimaudhui. Matokeo yanaonesha kuwa ujumi wa Kiafrika una athari chanya na hasi katika ujenzi wa wahusika wa kike. Kwa upande wa athari chanya, matumizi ya usimulizi, nyimbo, ngoma, maleba, majibizano, matendo na taashira yanawatofautisha wahusika kiutambulisho; yanamweka mwanamke katikati ya simulizi; na yanamjenga kama mzalishaji, mlezi, kiongozi, mwenye maarifa na mtetezi wa haki. Vipengele hivyo pia vinadhihirisha uwezo wa wanawake kushirikiana na kushiriki katika maendeleo ya jamii. Kwa upande wa athari hasi, vinamjenga mwanamke kama mhusika anayebebeshwa majukumu mazito ya kifamilia, anayenyanyaswa na mfumo dume, anayetazamwa kupitia mwili, anayekwamishwa na migogoro baina ya wanawake na anayenyimwa nafasi ya kutumia maarifa yake. Kushindwa kuisimamisha Nguzo Mama kunajenga taswira ya ukombozi wa mwanamke ambao haujakamilika. Makala inahitimisha kuwa ujumi wa Kiafrika katika Nguzo Mama si pambo la kisanaa pekee, bali ni nyenzo inayounda wahusika wa kike wenye uwezo, udhaifu na tajiriba zinazofichua migongano ya kijinsia, kiuchumi na kiuongozi katika jamii. Hivyo, wahakiki wa fasihi wanapaswa kutenganisha vipengele vya ujumi, sababu za matumizi yake na athari zake katika ujenzi wa wahusika.
- 3 October 2026
- Published by East African Nature and Science Organization in East African Journal of Swahili Studies
- Vol. 9 (3) , 428-440
Open AccessAthari za Ujumi wa Kiafrika katika Ujenzi wa Mhusika wa Kike katika Tamthiliya ya Nguzo Mama

- Vol. 9 (3) , 414-427
Maneno yanayochana: Matendo ya Kutishia Uso katika Mawasiliano ya Wahudumu wa Bodaboda na Abiria
Makala hii inachunguza namna waandishi wanawake wa Kiswahili wanavyojenga na kuwasilisha ubabedume (uanaume wa jadi au kibabe) kupitia wahusika wa kiume katika riwaya teule. Ingawa tafiti nyingi zimejikita katika usawiri wa wanawake ndani ya mfumo dume, nafasi ya waandishi wanawake katika kuibua na kuchambua ujenzi wa ubabedume imepewa uzito mdogo katika uhakiki wa fasihi ya Kiswahili. Kwa msingi huo, makala hii inalenga kubainisha vitambulishi vya ubabedume vinavyojitokeza katika riwaya teule na kueleza jinsi vinavyojengwa kupitia wahusika na mazingira ya kijamii wanamoishi. Makala hii imeongozwa na Nadharia ya Ubabedume ya Connell (1995) na imetumia mkabala wa kimaelezo wa uchanganuzi wa yaliyomo ya kifasihi. Data ilitokana na riwaya mbili za Kiswahili zilizoandikwa na waandishi wanawake – Yanarudia Tena (Himid, 2007) na Penzi la Damu (Manyanza, 2017), ambapo matukio, mazungumzo na tabia za wahusika wa kiume zilichanganuliwa kwa kuzingatia mihimili ya ubabedume. Matokeo yanaonyesha kuwa ubabedume hujengwa kupitia sifa kama mamlaka na udhibiti, mafanikio na hadhi ya kijamii, uthubutu na ukakamavu, kujitegemea na kutoonyesha udhaifu pamoja na jukumu la ulinzi na ukimu wa jamii. Aidha, ujenzi huu unaimarishwa na taasisi za kijamii kama familia, utamaduni na mila ambazo huendeleza matarajio maalumu kuhusu mwanaume halisi. Makala hii inahitimisha kuwa waandishi wanawake wanaitumia riwaya kama jukwaa la kufichua na kuhoji ujenzi wa ubabedume, wakionesha kuwa uanaume huo si hali ya kimaumbile bali ni zao la michakato ya kijamii na kitamaduni.
- 3 October 2026
- Published by East African Nature and Science Organization in East African Journal of Swahili Studies
- Vol. 9 (3) , 414-427
Open AccessManeno yanayochana: Matendo ya Kutishia Uso katika Mawasiliano ya Wahudumu wa Bodaboda na Abiria

- Vol. 9 (3) , 398-413
Ujenzi wa Ubabedume katika Riwaya za Kiswahili Zilizoandikwa na Waandishi Wanawake

Open AccessUjenzi wa Ubabedume katika Riwaya za Kiswahili Zilizoandikwa na Waandishi Wanawake